Radio MTV News
Februari 05, 2025
07:00 Jioni
Umoja wa Matifa watangaza kuwa watu zaidi ya elfu tatu walipoteza maisha kwakupigwa risasi Mjini Goma na uchunguzi bado ukiendelea
Februari 04, 2025
07:00 Jioni
Mashirika ya kiraia na asasi zisizo za kiserikali mashariki mwa DRC yasema kutokuona mabadiliko yoyote tangu yamefanyika marekebisho ya viongozi wa kijeshi katika ngazi zote uku waasi wakizidi kuzibiti miji muimu Kivu kaskazini na kusini.
Februari 03, 2025
07:00 Jioni
Raia wa mji wa Beni waandamana leo hii january 3,2025 kwaku pinga uvamizi wa jeshi la RWANDA na washirika wake wa M23. Hii ni baada ya mji wa Goma mji mkuu wa mkoa wa KIVU KASKAZINI kuangu mikononi mwa jeshi lwa rwanda RDF na waasi wa M23.
Januari 28, 2025
07:00 Jioni
Raia wa Mjini wa KINSHASA mji mkuu ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo waliandamana hii jumanne january 28,2025 kuonesha niya yao yakuunga mkono jeshi la CONGO FARDC linalo kabiliana na jeshi la RWANDA mjini goma,huku ekulu ya balozi wa ufaransa,rwanda,Ubeljiji,marekana na Uganda zikichomwa moto.
Januari 23, 2025
07:00 Jioni
Jeshi la Congo SADC na KIKOSI cha Umoja wa Matifa MONUSCO vimelazimika kutumia silaha nzito nzito na kuweka ulinzi mkali kwenye maeneo kadhaa kwa ajili ya ulinzi wa Mji wag Goma amba leo hii umetishiwa na waasi wa M23 ambao walichukuwa mji wa sake kwa saa za asubui na kembi ya kikosi cha SADC kilicheko Sake magharibi mwa mji wa Goma .
Januari 22, 2025
07:00 Jioni
Wasiwasi yaendelea kudhidi katika maeneo tofauti mkoani kivu Kaskazini na kusini hasa katika Miji ya Goma Na Bukavu baada ya waasi M23 kuudhibiti mji mdogo wa MINOVA; gavana wa kivu Kaskazini meja général PITER CIRIMWAMI aomba raia wa GOMA kutulia kwani serekali ya KINSHASA imechukua mikakati waku linda mji huo na raia.
Januari 16, 2025
07:00 Jioni
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ya adhimisha miaka 24 tangu auliwe raïs LAURENT DESIRE KABILA katika ekulu ya Urais jijini KINSHASA munamo january 16,2001.
Wananchi wa DRC waadhimisha kumbukumbu hio katika uzuni wakati pale rais Laurent Désiré Kabila alikua rais wa kwanza alie onekana kutumika kwa maslaha ya wa congo na maendeleo ya taifa lao. Laurent Désiré Kabila aliingia madarakani munamo mei 17,1997 baada yaku mukimbiza rais aliye kua na sifa ya udikteta barani afrika MOBUTU SESESEKO wazabanga hapo mbeleni rais wa jamhuri ya ZAÏRE.
Januari 15, 2025
07:00 Jioni
Jumuiya ya kikabila jimboni Kivu Kaskazini yaomba raia kuunga mkono juhudi za Jeshi la Congo FARDC na wapiganaji Wazalendo
Januari 09, 2025
07:00 Jioni
Serikali za Kenya na Uganda zimeanzisha mpango wa pamoja kutatua masuala ya mipaka ili kuimarisha ushirikiano katika shughuli za mipakani na kukomesha usafirishaji wa silaha haramu, uhamiaji haramu na mizozo ya maliasili miongoni mwa jamii zinazoishi karibu na mipaka.
Januari 08, 2025
07:00 Jioni
Jeshi la Congo DRC likishirikiana na wapiganaji Wazalendo wamefanikiwa kuwafurusha waasi wa M23 wanao pata msaada kutoka Jeshi la Rwanda tangu asubbui ya leo juma tano janwari 2025.
Januari 06, 2025
07:00 Jioni
Watu bado waendelea kuishi wasiwasi kubwa na wengine kukimbia makaazi yao kufatia mapigano kati ya jeshi la Congo FARDC na M23 ambayo serikali ya Kinshasa yasema wanaungwa mkono na jeshi la Rwanda.
Januari 03, 2025
07:00 Jioni
Waakzi wanao kimbia vijiji vyao mbali mbali kusini mwa wilaya ya Lubero waomba mkuu wa jeshi la Congo FARDC kuweke kambi yake pa Lubero kufatalilia kwa karibu operesheni za kijeshi, wakaazi hawa wanao hifadhi jina zao wasema hali ya kiutu ni mbaya kwasasa.
Desemba 30, 2024
07:00 Jioni
Watu sita wameuwawa na wengi kujeruhiwa pamoja na pikpiki kuchomwa moto na makaazi katika kata la Matombo Oicha wilayani Beni
Disemba 20, 2024
07:00 Jioni
Rais wa jamhuri yakidemokrasia ya congo, Félix Tshisekedi, ameunda upya jeshi la congo (FARDC).
Ni kupitia maagizo kadhaa yaliyosomwa kwenye televisheni ya taifa (RTNC) usiku wa Alhamisi Desemba 19, 2024 ambapo rais wa Nchi alichukua maamuzi makubwa ya kujaribu kurekebisha hali hiyo wakati nchi inapitia mgogoro na mvutano inayohusishwa na ugaidi wa wapiganaji wa Allied Democratic Forces (ADF) katika sehemu ya mashariki na kaskazini mashariki mwa majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri.
Wakati wa kusomwa, ilibainika kuwa Jenerali wa Jeshi Christian Tshiwewe, aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alibadilishwa na Meja Jenerali Jules Banza Milambwe . Jenerali Tshiwewe Christian, ambaye alibadilishwa, hata hivyo aliteuliwa kuwa mshauri wa kijeshi wa rais.
Meja Jenerali Tshitambwe Chiko ambaye hadi sasa alikuwa kamanda wa Operesheni za Kaskazini dhidi ya Vuguvugu la M23 na naibu mkuu wa jeshi anayesimamia operesheni na ujasusi aliteuliwa kuwa kamanda wa kanda ya kwanza ya ulinzi.
Disemba 16, 2024
07:00 Jioni
Wakaazi wa Vijiji vya Vutsorovya ,Alimbo wakimbilia katika Miji ya Kitsumbiro kuhufia mapigano makali kati ya M23 na jeshi la serikali FARDC ,kwenye vijiji vya Matembe .wakaazi wasema hali ni mbaya leo juma pili kwenye uwanja wa mapigano
Disemba 11, 2024
07:00 Jioni
Rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo FELIX TSHISEKEDI ahutubia wananchi kupitia Bunge na Seneti jijini KINSHASA hii jumatano Décember 11,2024.
Disemba 10, 2024
07:00 Jioni
Rais Mstaafu Wa Kenya Uhuru Kenyatta Amemshauri Rais William Ruto Kuwahusisha Wakenya Katika Shughuli Za Taifa, Ili Kuepuka Misukosuko Ya Kisiasa Inayoshuhudiwa. Wawili Hao Wamekutana Leo, Na Kujadili Maswala Muhimu Yanayolikumba Taifa.
Disemba 06, 2024
07:00 Jioni
Siku tano ya mapigano wilayani Lubero wakaazi walio baki katika nyumba zao pa kaseghe ,Chivako ,Kataro waomba msaada wa chakula kwani wana hofu ya kufia nyumbani kwa ukosefu wa chakula kutokana na mapigano kati ya M23 na jeshi la serikali maeneo haya.
Wakati huo huo hali yaendelea kuwa ya wasi wasi katika mji mdogo wa KIRUMBA Magharibi mwa wilaya ya LUBERO Kivu kaskazini,huku raia waki hofia pia maisha yao kwa sababu ya mapigano makali yanayo endelea hadi sasa.
Disemba 05, 2024
07:00 Jioni
Marekani kupitia shirika la USAID ukiwa ni shiriaka la wananchi wa Marekani kwa ajili ya Maendeleo laanza miradi nyingi kwa ajili ya afia Kivu kaskazini ,ikiwemo ujenzi wa vyoo na kunishinikiza usafi wa mazingira kupitia maji safi.
Disemba 04, 2024
07:00 Jioni
Watu tisa wauawa na wengine nne kujiruhiwa,hii na matokea ya shambulizi jipya la watu wenye silaha wanao dhaniwa kua ADF katika usiku wakuamkia hii jumatatu december,4 2024 katika mji mdogo wa OICHA kijijini BAKILA TENAMBO takriban kilometa 30 na mji wa Beni.
Disemba 03, 2024
07:00 Jioni
Jeshi La DRC Latangaza Kuzuia Jaribio La Shambulizi La Waasi Wa M23 Katika Kijiji Cha Matembe Wilayani Lubero Kivu Kaskazini
Novemba 27, 2024
07:00 Jioni
Wananchi wa maeneo mbalimbali nchini Tanzania leo wameshiriki zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku wito ukitolewa kudumisha Amani na kuwapa ushirikiano viongozi watakaokuwa wameshinda.
Novemba 26, 2024
07:00 Jioni
Shirika la P DDRCS nchini DRC laomba wapiganaji wote wanao shika silaha kusalimisha silaha zao kwa shirika hilo ili warudi katika maisha ya kawaida ,Kapuku Bwabwa William msimamizi wa taasisi hiyo kwa sasa asema muda umefika kwa kujenga amani , hii ni baada ya kukutana na gavana wa Kijeshi Meja Generali PETER CIRIMWAMI Mjini Goma
Novemba 25, 2024
07:00 Jioni
Rais William Ruto ameagiza Wizara ya Uchukuzi na Kawi kufutilia mbali mikataba iliyopendekezwa na Kampuni ya Adani Group ya kutwaa miundomsingi ya nchi katika sekta ya nishati na usafiri wa anga. mikataba hiyo ni mojawapo ya maswala yaliyowapelekea wakenya kuandamana.
Novemba 21, 2024
07:00 Jioni
Upinzani nchini jamhuri yakidemokrasia ya Congo ya pinga marekebesho ya katiba,hatua ambae ametangaza mwenyewe rais wa congo FÉLIX TSHISEKEDI huku wananchi wakiomba amani na usalama mashariki mwa nchi.
NOVEMBA 20, 2024
07:00 Jioni
Waziri mkuu wa TANZANIA Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wakubwa na wadogo kwenye sekta ya madini ili kuhakikisha wanaendesha shughuli zao kwa tija na kusaidia kukuza uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.
NOVEMBA 19, 2024
07:00 Jioni
Mashirika ya kiraia na wakaazi wa wa Eringeti na Kainama wilayani Beni waomba muungano wa jeshi la UPDF na FARDC ya Congo kuhudumisha usalama katika barabara Beni Bunia .hii ikiwa baada ya mashambulizi ya gari ya abiria.
NOVEMBA 14, 2024
07:00 Jioni
Wa fanya biashara huendeleya ku baki katika musukosuko katika Kijiji cha yakwa kwenye km 295 Na Muji wa buta Mutaani bazuele baada shambuliyo la wana biashashara wa wili walio uwawa kwa lisasi juma mosi iliyo pita.
Baada ya mauwaji hayo, maduka ya wa wana biashara wa Kabila la wanande yame Nyanyaswa na wakaazi waki pora vitu maduka. Mwandishi wetu mbanusi mutumwa ame zungumuza kwa njiya ya simu Na kiongozi makamu wa shirika la wana biashara
NOVEMBA 11, 2024
07:00 Jioni
Inspekta jenerali wa polisi nchini kenya a amekanusha kuhusika kwa polisi katika visa vya utekaji nyara nchini humo.
NOVEMBA 07, 2024
07:00 Jioni
Mlio wa risasi ulisikika leo usiku katikati mwa Mji wa Beni Kivu laskazini taarifa ya vyombo vya usalama zasema ni majambazi wenye silaha waliendesha shughuli zao usiku wa Novemba 6 hadi 7 katika vitongoji vya Malepe na Rwangoma katika mtaa wa Beu mji wa Beni.
NOVEMBA 06, 2024
07:00 Jioni
Jeshi La Congo FARDC La Tangaza Kuwa Shika Wapiganaji Mai-Mai 12 Mashariki Mwa Jamhuri Yakidemokrasia Ya Congo Wilayani Mambasa, Katika Mkoa Wa Ituri
NOVEMBA 05, 2024
07:00 Jioni
Naibu rais wa Kenya Kithure Kindiki ameanza majukumu yake rasmi leo alipojiunga na Rais WilliamsRuto katika Mahakama ya Juu, wakati wa kuadhimisha miaka 12 tangu mahakama ya juu zaidi nchini kuanzishwa.
NOVEMBA 04, 2024
07:00 Jioni
Kume ripotiwa kuunguzwa kwa nyumba zaidi ya 300 ya raia wilayani saké takriban kilometa 20 na mji wake huko raia wakitishia kurudi maeneo ambao wame kimbia hata kama kuna vita kwani wame teseka siku nyingi katika kambia pasipo musaada wa serekali.
NOVEMBA 01, 2024
07:00 Jioni
Muungano wa kanisa katholika nchini DRC wapinga hatua ya serikali kutaka kufanya marekebisho ya katiba.