Habari

Waziri Wa Maji Tanzania Amuondoa Mkandarasi Mradi Wa Maji Kazuramimba Nakuagiza Mwezi Mmoja Wananchi Wapate Maji

JULAI 20, 2023
Border

Kazuramimba-Uvinza-Kigoma

Waziri wa Maji nchini Tanzania Mhe.Jumaa Aweso amekasirishwa na kitendo cha mradi wa Maji Kazuramimba Uvinza Kigoma kuchukua muda mrefu bila kukamilika huku wananchi wakiendelea kuteseka na ukosefu wa huduma hiyo muhimu.

Awali changamoto ya Mradi wa Maji Kazuramimba ilikua ni kuchelewa kwa Tanki la Maji ambapo mwaka jana Waziri Aweso alifika na kuhakikisha Tenki linatoka na kufika Uvinza Kigoma.

Waziri Aweso amefanya maamuzi ya kumuondoa Mkandarasi wa Mradi wa Maji Kazuramimba unaotekelezwa kwa Ufadhili wa Enabel na Mkandarasi akiitwa Nangai Engineering Company Limited baada ya kutembezwa umbali mrefu bila kuona vituo vya Maji akiongozana na wananchi wenye hasira kali.

Wakati wa ziara hiyo Waziri hakuridhishwa na kasi ya Mkandarasi katika utekelezaji wa mradi huo ambao umeanza toka Novemba, 2020 na alitakiwa kukamilisha kazi katika kipindi cha miezi tisa na badala yake sasa ni mwaka wa tatu.

Kutokana na hali hiyo Waziri amemundoa kufanya kazi hiyo, ameivunja kamati ya Maji ya Mradi huo na kuitaka RUWASA kukamilisha mradi huo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na kuusimamia.

Oliver G Nyeriga -MTV TANZANIA