Tanzania

Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Atoa Siku 7 Watendaji TARURA, DAWASA Kukamilisha Barabara Muhimbili

JULAI 24, 2023
Border
news image

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewapa siku saba Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Mikinga na Mkurugenzi wa Usafi wa Usimamizi wa Usafi wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingiza (DAWASA) Lydia Ndibalema wawe wamekamilisha kipande cha barabara ya Mariki kinachoingia geti kuu la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kiwango cha lami.

Barabara hiyo ambayo ilibomolewa kwa urefu wa mita 60 kupisha matengenezo ya bomba la maji machafu linalotoka katika hospitali hiyo ilipaswa kuwa imekamilika mwishoni wa mwezi wa sita 2023.

Oliver G Nyeriga