DRC Ituri

Watu Zaidi Ya (13 ) Kumi Na Tatu Wauwawa Na Wengine Kujerihiwa Miongozi Mwao Watoto Sita Wapoteza Masiha Kwenye Vijiji Vya Tchomia Mkoa Ituri Kaskazini Mashariki Mwa Congo

JULAI 23, 2023
Border
news image

Vyanzo vya usalama hasa jeshi Mkoani Ituri vimesema ,watu Zaidi ya kumi na tatu (13 ) wameuwawa na kundi lenye silaha lisilo julikana ,miongoni mwa watu walio uwawa kuna watoto sita katika Vijiji vya Tchomia Mkoni Ituri ambako mara kwa mara kumekuwa kukiripotika hali mbaya ya ukosefu wa usalama, baadhi ya wilaya ya Ituri kumekuwa kukiripotika mauaji ya raia wasio kuwa na hatia n ahata nyumba na vijiji vya watu kuchomwa moto Zaidi ya miaka miwili sasa ,japokuwa Mkoa huo upo chini ya uongozi wa kijeshi lakini hali bado kutulia.

Ituri ni mkoa wenye madini mengi Kaskazini mamshariki mwa Congo lakini bado wananchi wake wakiendelea kuteswa kutokana na madini yao kwa vita wasio fahamu sababu. Vijiji vya Tchomia katika eneo la chifu la bahema banywagi kwenye pwani ya ziwa albert katika eneo la Djugu kilomita 65 kusini magharibi mwa Bunia.ndio kumeshudiwa machafuko makubwa na kupelekea wakaazi wengi kukimbilia hata taifa Jirani la Uganda wakitumia ziwa Albert.

Askari wa kikosi cha wanamaji walieko eneo hiyo ya Gobu wanasema walilazimika kufyatua risasikujaribu tuliza hali kufatia hathira ya wananchi wanao kuwa na hathira kuona ndugu zao kuwawa kila siku bila hatua Madhubuti ya ulinzi.

MTV/ BUNIA