DRC

Watu Mashuhuri Kutoka Vijiji Vya Rugari Wilayani Rutshuru Watangaza Wasiwasi Wao Kuhusu Elimu Ya Watoto Wao Katika Kipindi Hiki Cha Vita Vya M23 Wengi Wakiwa Kambini

JULAI 31, 2023
Border
news image

Suala la usalama na kibinadamu katika eneo la Rugari, kichifu Bwisha wilayani Rutshuru imekuwa miongoni mwa sababu kubwa lililo pelekea watu mashuhuri wa Rugari kuendesha kikao Jumapili hii, Julai 30 katika Mji wa Goma. Akiwa miongoni mwa waandalizi kiongozi wa Kiasili Erick Mashagiro asema hali ni mbaya hasa wasiwasi kuhusu elimu ya Watoto wadogo wa shule ambao mwaka mmoja sasa hawaendi shuleni kutokana na vita vya M23 . Éric Mashagiro, kiongozi wa eneo hili la Rugari asikitika kwa hali ambayo yaendelea kwenye vijiji vyake cha vita vya M23. Chanzo chetu cha habari kinataka kuona watoto wa shule walio katika kambi mbalimbali za IDP na waliokaa Rugari waliokosa mwisho wa mwaka wa shule, waweze kuendelea mwakani.

“Sisi sote ni wahanga wa vita hivi lakini watoto wetu ambao hawasomi ni wahasiriwa zaidi. Hawakusoma mwaka ulio malizika na kufikia Septemba ni kurudi shuleni kwa mwaka mpya. Vipi kuhusu watoto wetu walio baki katika kambi za IDP na wale waliobaki Rugari bila elimu? Akisisitiza Éric Mashagiro, kiongozi wa vijiji vya Rugari "Wacha wote wanaopanda ugaidi wafikirie elimu ya watoto wetu" anasema.

Vigogo hawa mbalimbali wa Rugari pia wameitaka serikali kutowanyima haki zao ya kikatiba ya kushiriki Uchaguzi ili wawe na wawakilishi Bungeni.

Ni tangu Oktoba 2022 Shule zote zilisitishwa katika katika eneo la Rutshuru, ikiwemo Rugari. Wanafunzi walizuiliwa kwenda shule kufuatia uwepo wa waasi wa M23 katika eneo la Rutshuru ,Msisi na sehemu moja ya nyiragongo pamoja na kuhama kwa idadi kubwa ya watu ambao ni wakimbizi kwa sasa.

Aline Kataliko