DRC

Watu 1006 wameuwawa wilayani Rutshuru, Masisi na Nyiragongo tangu tarehe 13 juni, 2022, hadi 26 Julay 2023 yasema muungano wa wanusurika wa vita Kivu Kaskazini

JULAI 26, 2023
Border
news image

Muungano wa wathiriwa wamewasilisha malalamiko dhidi ya kundi la wa M23 katika ofisi ya muendesha mashtaka ya kijeshi ya jimbo la kivu kaskazini hii tarehe 26 julay 2023.

Jean Claude Mwamba Mwana sheria wa muungano huu ameomba sheria ya kongo kufanya kazi yake na kusaka waalifu na watu walio sababisha mauwaji kwa umbali ama kwa karibu.

Utafahamu kwamba M23 inadhibiti sehemu kubwa ya wilaya ya Ruthsuru,Masisi na Nyiragongo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu mapigano kati yao na jeshi la serikali nakupelekea maelefu ya wakaazi kukimbia vijiji vyao n'a kuwa wakimbizi wa ndani katika kambi ambako wapitia hali ya mateso na ubakaji.

Ya Michombero/Ruth Alonga