DRC - Uvira

Usafiri kati ya Jamuuri ya kidemokrasia ya Congo Na nchi jirani za Ukanda wa Maziwa Makuu Na Afrika ya Mashariki umebweteka jumanne julai 25 Kutokana Na Mgomo Baridi wa wanainchi ulioitishwa Na shirika jipya la Raia.

news image

Akizungumuza na MTV kwa njia ya simu mkaazi alie hifadhi jina lake amesema hali kwa sasa Imakuwa Tulivu baada ya maandamano yah apo jana juma nne kuonyesha Asira Zao za kutokujengwa kwa Barabara yakiukanda na kusumbuliwa na polisi wa barabarani .wakaazi wakishutumu serikali ya sasa na ilio pita kushindwa ujenzi wa barabara Muhimu inayo unganisha DRC na Burundi ikiunganisha na Tanzania.

Uvira inapakana mkoa wa Kivu kusini ikipakana na taifa la Burundi Na Tanzania.

Wasafiri wengi walichelewa Safari Zao kwa njia ya Barabara Na usafiri wa maji katika ziwa Tanganyika,Maboti Pia yalisitisha kwa mda Safari Zao kuitikia wito wa mashirika ya kiraia.

Baadhi ya wa safiri wa kutoka Uvira kwenda Burundi Na Miji Mingine Jirani kama vile Bukavu na Baraka walilazimika kuondoka Mjini Uvira adhuuri ya Siku moja kabla ya mgomo huo.

Ni tangu Alfajiri Mapema Adi jioni ya jumanne iyo Shuguli zote zikiwa zimefungwa isipokiwa Duka za Kuuza dawa.Miji Ya UVIRA,Sange,Kiliba na Mingineyo,Ndiko kumechachamaa mgomo huo.Magogo,moto,Na mawe yaliwekwa Barabarani.

wanainchi walitaka kila mtu atembee kwa miguu Siku iyo ili kujionea jinsi gani Imebomoka Na kuaribika Barabara ya taifa namba Tano.Barabara iyo inaziunganisha inchi za Drc,Rwanda,Burundi Na zambia.

Kulingana naye Masimango Mafikiri mratibu wa shirika jipya la Raia lengo la Mgomo Huo ni kuonyesha serikali kwamba ahadi nyingi zisizo timizwa ni kutibuwa wanainchi.

Katika mgomo huo uliosindikizwa Na maandamano kumeripotiwa Na utovu wa nidhamu wa waandamanaji haswa maeneo ya Kasenga Na kwenye Daraja la moto Mulongwe.Wapitaji KADHAA wasema kubuguzwa na waandamanaji.Wakiwa Na mabango , waandamanaji walijielekeza kwenye ofisi ya meya wa mji Na kusoma risala yao.

Mamlaka ya mji yamewaaidia kufikisha malalamiko yao kwenye ngazi za juu.

Mji wa Uvira ni Mji ulio Na Bandari ya pili kuingiza mapato Mengi serikalini Bahada ya Bandari ya Matadi.

Thomson undji Batangalwa William MTV, UVIRA.