Tanzania

Tuondoe Tofauti Zetu Kufikia Maendeleo Ya Kweli- Kikwete

JULAI 24, 2023
Border
news image

Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani kikwete wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Bwilingu na Ubena kwa nyakati tofauti akiwasisitiza kuyakimbilia maendeleo zaidi ili nchi isonge mbele.

Mbunge huyo ameyasema hayo baada ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa katika jimbo hilo na kuongea na wananchi baada ya ukaguzi.Katika ziara hiyo Mhe.Kikwete amezindua program ya ukusanyaji taka yenye lengo la kutengeneza mazingira na kufanya Mji wa Chalinze kuwa msafi na baadae kukagua ujenzi wa Mabweni, Zahanati kabla ya kuzungumza na wananchi katika kijiji cha Ubena Zomozi na baadae Lulenge katika kijiji cha Kaloleni mjini hapo.


Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania