TANZANIA

TP Mazembe Ziarani Mjini Kalemie Mkoani Tanganyika Kwa Maandalizi Ya Msimu Mpya

JULAI 29, 2023
Border
news image

Klabu ya Moise Katumbi mmoja kati ya jewafanya siasa nchini TP MAZEMBE imewasili mjini Kalemie leo jumamosi 29 Julai 2023 kwa ziara ya siku Tano.

Ujio wa klabu hiyo ni moja ya utalii na kujiandaa kwenye mashindano mbalimbali yakiwemo ya kitaifa, na kimataifa kwenye msimu ujao.

TP Mazembe wataiwakilisha nchi ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwenye mashindano ya mabingwa barani Afrika baada ya maamuzi ya tume ya michezo ya CONOR iliyo teuliwa na FIFA kusimamia michezo kwa muda nchini Kongo kuamua msimamo wa ligi ya taifa (LINAFOOT) iamuliwe kufuatana na matokeo ya misimu minne iliyopita, swala lililowapa TP Mazembe kuibuka washindi baada ya mechi za mzunguruko wa kwanza kushindwa kumalizika.

TP Mazembe watacheza mechi ya kirafiki jumapili hii ya tarehe 30 Julai 2023 na klabu itakayoundwa na wachezaji watakaochaguliwa na uongozi wa michezo mjini kalemie kutoka kwenye vilabu vya hapa kalemie.

Akiongea na MTV mjini kalemie, kocha wa TP Mazembe msenigali Lamine Ndiaye amesema wamekuja hapa kwaajili ya kuwapa raha maefu ya mashabiki wao wanaopatikana jimboni Tanganyika na sio kuwekea maanani mechi ya jumapili hii.

Kabla ya Mazembe kufika hapa Kalemie, walifanya ziara pia uko katika mji wa Kamina jimboni Haut Lomami ambako walicheza na klabu iliyokua na mchanganyiko wa wachezaji na kuwafunga mabao 7-0.

Ally Zuberi MTVDRC/Kalemi