DRC

TP Mazembe Waonesha Ubabe Mjini Kalemie

JULAI 30, 2023
Border
news image

Mechi iliyokua inasubiriwa kwa hamu na maelfu ya watu mjini kalemie hatimae imechezwa leo jumapili tarehe 30.07.2023.

Mechi hiyo baina ya vijana wa mjini kalemie wakicheza na Moja kati ya klabu Bora nchini na Afrika kwa ujumla TP Mazembe ilipigwa katika uwanja wa Joseph Kabila Kabange (JKK) leo mjini kalemie katika Jimbo la Tanganyika.

Mechi iliyochezwa mbele ya maelfu ya mashabiki ilikua na shamrashamra za kipekee huku mashabiki wakishamgilia mwanzo mwisho baada ya kuwaona baadhi ya nyota wa klabu hiyo.

Mmoja kati ya watu walichukua hisia za watazamaji ni Robert Kidiaba ambaye mashabiki walimtaka aoneshe mbwembwe zake na kuzionesha jambo lililofurahisha mashabiki waliofika uwanjani.

Dakika 8 za kipindi cha kwanza zilitosha kwa Mchezaji Augustine OLADAPO wa TP MAZEMBE kupata bao la kwanza Ikiwa ni muda huohuo ndipo mwanasiasa maarufu nchini na mmiliki wa klabu hiyo Moise Katumbi aliingia uwanjani.

Hadi dakika 45 za kipindi Cha kwanza Tp Mazembe walikua wanaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Kalemie

Dakika ya 51 Mchezaji hatari wa TP MAZEMBE Philippe Kinzumbi alipiga mkwaju hatari ulio wapa Mazembe bao la pili

Muda mfupi Mchezaji wa TP Mazembe alioneshwa kadi nyekundu na kusababisha Mazembe kucheza Pungufu.

Mechi ilizidi kuwa na ubora zaidi pale Tp Mazembe waliendelea kuonesha mpira wa kimataifa kwa kurandaza pasi mara kwa mara wakiendelea kulisakama lango la vijana wa Kalemie.

Dakika ya 71, Mchezaji wa TP Mazembe alichezewa rafu katika eneo hatari na kupewa penalti iliyowekwa kimyani ni mchezaji Fily TRAORE.

Hadi dakika 90 Zinakamilika katika uwanja wa JKK mjini kalemie, ubao ulisomeka Kalemie 0-3 Tp Mazembe

Mashabiki waliopata nafasi ya kuongea na MTV wamefurahi na ujio wa Mazembe huku wakisema wanafurahi kwa matokeo hayo maana walifika uwanjani wakiwa na fikra ya kufungwa mabao zaidi ya 5.

TP Mazembe wataendelea kujiandaa kwa mechi mbalimbali hapa nchini huku duru zingine zinadai kuwa kituo kinachofuata ni GOMA Kisha Bukavu.

Ally Zuberi MTVDRC Kalemi