DRC

Serikali Ya Ujeremani Yatangaza Ushirikiano Wake Na Serikali Ya Congo Kupitia Wizara Ya Ushirikiano Wa Kikanda

news image
MTV
JULAI 25, 2023
Border
news image

Akizungumuza na Waziri wa ushirikiano wa kikanda Mabusa Nyamwisi kwenye Osifi yake Mjini Kinshasa balozi mdogo wa Ujerumani asema kwa sasa taifa lao limejipanga vilivyo kusaidia taifa la DRCongo kurejesha Amani ,utulivuna usalama mashariki mwa DRC ambako Hali ya kibinadamu ni ya kushangaza katika sehemu hii ya Jamhuri inayokumbwa na uasi wa M23 unaoungwa mkono na Rwanda.

Mheshimiwa LARS MEYLANN, Julai 25, 2023, alijadiliana na Waziri wa Ushirikiano wa kikanda, Mbusa Nyamwisi kuhusu uwezekano wa kuleta amani eneo hili kwa njia ya Diplomasia.

Ikumbukwe kwamba ushirikiano wa Ujerumani na DRC unaungwa mkono katika secta ya maendeleo kwa kusaidia wathirika wa unyanyasaji wa kijinsia. Berlin pia inafanya kazi kwakuweka utaratibu katika biashara ya madini mbali mbali inayo kuwa chanzo cha machafuko ,hasa, dhahabu, shaba na cobalt.

MTV