Habari

Tanzania
Serikali Ya Tanzania Na Wadau Kuungana Kupata Ufumbuzi Tatizo la Ajira

JULAI 21, 2023
Border

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau imekusudia kuanzisha Mradi wa kutatua changamoto ya ajira kupitia Mradi wa vituo vya kuuzia chakula utakaowawezesha Vijana kujiajiri ili waweze kuepuka kushiriki Matukio Matendo maovu.

Akizungumza wakati wa kikao kazi na Watumishi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na Makundi Maalum kutoka Tanzania pamoja na Wizara nyingine za kisekta, Mkurugenzi wa Kampuni ya X-NIHILO Paul Mashauri amesema mradi huo utawainua vijana wengi na kuwaondoa kwenye msongo wa Mawazo linalowakumba vijana kwa kukosa vipato.

“Ili kijana aweze kunufaika na mradi huu inabidi awe ni kijana mwenye maadili na hilo litathibitishwa na Wanajamii kwakuwa fomu zakujiandisha zitatolewa na ofisi ya mtendaji kata na watu watahojiwa ili kubaini mwenendo na Maadili ya kila mtu

Akizungumza Kwa niaba ya Wanasheria kutoka wizara za Kisekta ambao walialikwa kwa ajili ya kutoa ushauri juu ya mradi huo, Wakili Happiness Msimbe kutoka wizara ya Maendeleo ya jamii ,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha mradi huo unatimia na kutekelezeka kote nchini.