DRC

Rais wa Congo DRC Félix Tshisekedi afungua Rasmmi michezo ya Olimpik U awamu ya 9 Mjini Kinshasa

JULAI 29, 2023
Border
news image

Ni awamu ya TV 9 ya michezo za Olimpiki zinazo leta pamoja mataifa zinazo tumia kifaransa kama lugha rasmi Duniani. katika hotuba yake Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) Ijumaa Julai 28 katika jiji kuu la Kinshasa, Felix Tshisekedi alisema:

"Nina furaha tele kupokea wazungumza kifaransa tokea mataifa mbalimbali Duniani, kwa miyadi hii ninayo chukulia kama fursa ya kipekee kwa mataifa yanayo tumia kifaransa kama lugha rasmi kwa kufahamiana vizuri, fursa kwa taifa la Kongo kuonyesha uwezo iliyo nawo kimichezo na kitamaduni. Michezo hii ya olimpiki ni ishara ya ukaribu wenu kwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, heshima yenu kwa taifa hili pia utekelezwaji wenu wa malengo ya jumuiya ya mataifa yazungumzayo kifaransa, nchi ya Kongo Kinshasa ikiwa moja wapo. Nchi yetu ita endelea kutoa mchango wake kama Taifa la Pili Dunia la kifaransa baada ya Ufaransa, kuhusu idadi ya wanao zungumza lugha ya kifaransa nchini, idadi itapanda zaidi ifikapo mwaka 2050. Kuhusu kazi ya kuboresha jumuhia yetu, nawa hakikishia kwamba Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, iko pia kwenye mustari wa mbele kujenga jumuiya" alisema Felix Tshisekedi raisi wa Taifa ya Kongo.

Ni vema kukumbusha hapa kwamba michezo hii ya Olimpiki ita dumu kwa muda wa siku 9, yaani hadi Ogasti 6, 2023. Kuna aina 6 ya maonyesho ya michezo miongoni, ni mchezo wa vikapu kwa wanawake, mpira wa miguu kwa wanaume chini ya miaka 20, mbiyo za sakafu, mbiyo za baiskeli

Eriksson LUHEMBWE