DRC

Mwanamziki Mbilia Bel Awasili Goma Kivu Kasakazini Kwa Tamasha Ya Kuungana Na Watu Wanao Tesekea Na Vita Mashariki Mwa Congo

JULAI 31, 2023
Border
news image

Mwanamziki mbilia Bel yuko Goma tangu jioni hii ambako anakuja kuendesha tamasha kubwa linalo lenga hadi za kiutu na kujiunga na watu wanao pitia matatizo ya kivita Pamoja na kutakia amani kwa wanawake na Watoto mayatima wa wanajeshi wanao pambana mustari wa mbele.

Namnukuu: "nafurahishwa kuwa karibu na ndugu zangu wa Goma ,kwa siku mbili nitaangalia namna ya kusaidia wanawake wa wanajeshi Pamoja na wanajeshi wenyewe wanao kuwa kwenye mapigano ili wafahamu kwamba tupo Pamoja nao:>>mwanamziki huyo amekutana na Gavana wa Kivu Kaskazini Luteni Generali Constant Ndima Kongba.mwanamziki amesema wa Congo wana taifa moja ambalo ni Congo DRC lazima kulipenda. Congo ni yetu na amani haina Bei ,bila amani hakuna lolote ambalo laweza kuendelea lazima watu wote kuchangia amani na usalama."

Mbilia Bel amesema mwaka wa 2023 lazima uwe mwaka wa amani,na usalama na mshikamano,mwanamziki huyu anasema kwa sasa anawafunza wasichana wengine ili waendelee na bendi yake siku zijazo.

Muhongya Bwambale - MTV