TANZANIA

Mkoa Wa Kigoma Waadhimisha Siku Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi Maweni

news image
MTV
JULAI 26, 2023
Border
news image

Mkoa wa Kigoma umeadhimisha Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma -Maweni

Maadhimisho hayo yamefanyika July 25, 2023 yakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ambapo amewataka Wakazi wa Mkoa huo kujitoa kulitumikia Taifa kwa uzalendo kama Mashujaa waliotangulia

Amewataka Wananchi wa Mkoa huo kuendelea kushiriki shughuli za usafi katika makazi na maeneo yao ili kuepukana na magonjwa na kujenga utamaduni wa uwajibikaji binafsi katika kutunza Mazingira na kujikinga na maradhi.



Zoezi hilo la usafi limehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Kamati ya Usalama Ulinzi na Usalama, Uongozi wa Hospitali ya Rufaa (Maweni), Watumishi pamoja na Wananchi

Tanzania huadhimisha Siku ya kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kuulinda Uhuru wa Tanzania kila ifikapo Julai 25, kila mwaka. Siku hii huambatana na kushiliki shughuli mbalimbali za kijamii

MTV