HABARI

Makamanda 2 Wa ADF Wameuawa Na Majeshi Ya Muungano Fardc UPDF Wilayani Beni

JULAI 31, 2023
Border
news image

Vikosi vya muungano vime fanyikiwa pia kunyanganya siraha 5 bondeni Muhalika wakati wa operesheni , kilomita 80 kusini mashariki mwa jiji la Beni usiku wa kuamkia leo juma tatu ya Julai 31 , amesema msemaji wa operesheni Shujaa.

Kanali MAK HAZUKAY
"Na dhibitisha kwamba baada ya shambulizi ya kushitukiza, tuli gundua maiti ya magaidi wawili wa ADF , wanaonekana kama ni makamanda ila tuna endelea kuwa chunguza kati yao kuna mwanamuke . Ila opersheni ina endelea hakuna ambaye alitangaza mwisho wa operesheni ya kusafisha Muhalika , ni kazi inayo hitaji mda na kuendeshwa polepole tena na uhakika , ili kuzuia adui kufanya vitendo vibaya baadaye , sababu bonde la Muhalika ni maskani kubwa ya Adui anapo jipatia pia chakula , ni kugumu kufanya kazi nzuri sehemu zingine kama hatujazibiti kikamilifu Muhalika"

Erickson Luhembwe - MTV BENI