Habari

Tanzania
Maelfu Ya Wakaazi Wa Goma Watembea Mitaani Na Katika Baadhi Ya Barabara Kutafuta Maji Ziwa Kivu

JULAI 27, 2023
Border
news image

Nitangu usiku wa leo sehemu kubwa ya wakaazi wa Mji wa Goma wanawake ,vijana wasichana na wamama wameonekana na jerekani mitaani na katika baadhi ya barabara kutafuta maji hapa na pale ,baada ya maji kukosa nyumbani kwao.

Wakaazi hao washangazwa kuona Mji wa Goma ulieko pembeni ya ziwa Kivu wakazi wake waishi katika tatizo la ukosefu wa maji safi kila mara.hii ikiwa sio ya mara ya kwanza hali kama hii kutokea Mji Goma ,Mji wa kitalii unao patikana mpakani na taifa la Rwanda eneo lake la mashariki ,ziwa Kivu eneo lake ka kusini,mbuga la Virunga eneo lake la kaskazini na wilaya ya masisi eneo lake la Magharibi.Mji mzuri sana ambao kwa sasa unau meme kutoka bwawa la Virunga,SNL na Nuru inayo tumia sola, lakini maji ikiwa tatizo shugu kwa wakaazi katika baadhi ya kata.

Taasisi ya maji REGODESO inayo shughulikia na kuwapa maji wakaazi wa Goma yasema kwamba kuna tatizo kidogo za kiufundi ambazo zafanyiwa kazi kwa sasa. Maji ikiwa muhimu kwa mwanadamu na shughuli zote za Maisha wakaazi waomba shida hii kutatuliwa kwa haraka hasa Mji wa Goma ukiwa unazunguukwa na kambi nyingi za wakimbizi ambazo zikikosa maji inaweza kuwa shida kubwa.

AM/MTV DRC