Habari

Tanzania
Jeshi La Polisi Kanda Maalum Ya Dar Es Salaam Nchini Tanzania Linamshikilia Mohamed Jabiri

JULAI 21, 2023
Border
news image

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania linamshikilia Mohamed Jabiri mwanafunzi wa shule ya sekondari Qiblaten Kawe, Wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kumuua mwalimu wake (patron) Hassan Mohamed (21) baada ya kumshambulia kwa kisu shingoni na baadae kupoteza maisha.

Mtuhumiwa huyo alitekeleza mauaji hayo Julai 20, 2023 saa 11:10 alfajiri baada ya kumshambulia mwalimu (Patron) aliyekuwa akiwahimiza wanafunzi wakati huo kuhudhuria ibada ya alfajiri.

Majeruhi alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na mwili wake umehifadhiwa Hospitali hiyo.

Mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi za kisheria.

Imetolewa na ;
Muliro J. MULIRO - SACP
Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam Tanzania.

Oliver G Nyeriga - MTV TANZANIA