DRC

Jeshi La Jamuuri Ya Kidemokrasia Ya Congo Lajipiga Kifua Kuwapa Kichapo Magaidi Kutoka Kundi Wa ADF Mkoani Ituri

JULAI 25, 2023
Border
news image

Macky Hazukay Msemaji wa operesheni za kivita zinazoendeshwa kati ya jeshi la kongo Na la Uganda amesema kwamba juma hili Gaidi Mmoja Kutoka kundi la kihalifu la ADF ameuwawa Na jeshi la Congo FARDC wakati wa operesheni kali walioiendesha usiku wa julai 24 kucha 25 kijijini Ndalya Tarafani Irumu kwenye mpaka wa Ituri Na Kivu kaskazini.

Kulingana Na Msemaji huyo ni kwamba silaa moja nzito,Radio za mawasiliano ya kijeshi Na dhana zingine nyingi za kivita,zimetekwa Na FARDC katika operesheni izo zilizo rindima Magaribi Mwa Barabara ya kitaifa namba nne.Jeshi lime akiki kuwa lengo la operesheni izo ni kuzidisha ulinzi wa wanainchi katika eneo lote la Eringeti-Kainama

Tchabi Adi - Bunia