DRC/LUBERO

Jeshi La Congo FARDC Latangaza Kuwa Waua Wanamgombo 4 Kutoka Kundi La Mai Mai Wilayani Lubero Kivu Kaskazini Mashariki Mwa Congo

JULAI 23, 2023
Border
news image

Katika Tangazo lilo tolewa nae Antony Mualushayi, msemaji wa operesheni ya SOKOLA 1. Nikwamba wapiganaji nne (4) kundi wapiganaji wa chini kwa chini Mai Mai wameuwa wakati wa mapigano ilio dumu dakika ishirini kwenye vijiji vya Vurondo wilayani Lubero ,na jeshi la serikali kufanikiwa kuteka Ngome muhimu ya wapiganaji hao Antony Mualushayi akisema.

Antony ameongeza kuwa mbali na muwaua wapiganaji inne selah ana vifaa vingine vya jeshi na polisi vilichukuliwa toka mikoni mwa wapiganaji hao.

news image

Kapteni Antony Mualushayi, ameongeza kwamba jeshi la serikali FARDC liliendelea kutekeleza operesheni za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao ambao wengi wameombwa kuingia katika mchakato wa PDDRC-S, ikiwa ni mpango wa serikali wakupokonya silaha wapiganaji wote kwa ajili ya kurejesha amani na Usalama mashariki mwa Congo.

Mpango ulioanzishwa na serikali ya Kongo. Viongozi wa PDDRC-S wakiomba makundi yenye silaha kusalimisha silaha kwa serikali ili wachague Maisha mengine kuliko ya silaha kwani wanao teseka ni Raia wasio kuwa na hatia hasa wana vijiji ambao wengi hulazimika kuhama makaazi yao na kuwa wakimbizi katika taifa lao.

Mtv DRC