DRC - Michezo

Wachezaji kutoka mataifa 40 inayo zungumuza Lugha ya Kifarasa (Francophonie) waanza kuwasili Mjini Kinshasa kwa maandalizi ya michezo mbali mbali itakayo anza tarehe 28 mwezi huu

JULAI 24, 2023
Border
news image

Kwenye ukurasa wake wa Twitter Patrick Muyaya kwenye Msema ji wa serikali ya Congo DRC amema maandalizi ya kuwapokea wachezaji na wadau wengine watakao shiriki michezo ya « Francophonie » yanaendelea vizuri Pamoja na ujenzi wa makaazi itakayo wahifadhi ,na usalama ukiwa tele Kote Mjini Kinshasa ambako jumuhia ya ulimwengu wa kifaransa,inatarajiwa kuwasili na wanegine wakiwa tayari wameanza kuwasili na kuanza mazoezi kabla ya michezo kuanza Ijumaa Julai 28.

Kwaida mataifa wachezaji kutoka mataifa 40 yanatarajiwa kushiriki michezo mbali mbali Mjini Kinshasa .

Rais wa Congo Felix Tshisekedi alisema Congo imejipanga vilivyo kwa mapokezi ya wageni wote nchini hasa Mjini Kinshasa ambao watashiriki michezo ya francophonie

Serikali ikipongeza waandalizi wanao fanya kazi usiku na mchana kwa kufanikisha michezo hiyo ambayo itavutia vijana na watu wazima.

Michezo kama hii ilifanyika Abidjan nchini Ivory Coast mnamo 2017 ,na leo Congo DRC itapata bahati ya kupkea Ghafla kubwa Barani Africa .kamati ya mapokezi ikiomba wakaazi wa Mji wa Kinshasa hata kutoka mikoa mbali kuwapokea Vizuri wageni wote watakao kuja kushiriki Michezo ,nafasi 80 000 zikiwa zimeandaliwa .

Mamlaka imeahidi sherehe kubwakufanyika , na wasanii maarufu kutoka Ngomba za DRC wakiwa wamejipanga kudumbuiza wageni.

Hili litakuwa toleo la kwanza kuandaliwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Licha ya wasiwasi fulani , DRC inafanya juhudi kuandaa Michezo hii ambayo iko chini ya ishara za matumaini na mshikamano wa ulimwengu unaozungumza Kifaransa.

Ruth Alonga