Tanzania

Dk. Mpango Awaomba Watanzania Kuombea Viongozi Waongoze Nchi Kwa Kuzingatia Amani Na Umoja

JULAI 24, 2023
Border
news image

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 24 Julai 2023 ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba Jimbo Kuu Katoliki Songea katika Ibada ya kawaida ya asubuhi.

Akiwasalimu waumini mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Makamu wa Rais amewapongeza wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa miradi mingi ya maendeleo pamoja na kuupongeza uongozi wa mkoa huo kwa usimamizi mzurii wa miradi hiyo.

Makamu wa Rais amewaomba waumini na viongozi wa dini kuendelea kuombea taifa na viongozi wake ili kuweza kutambua ukuu wa Mwenyezi Mungu wakati wote wanapolitumikia Taifa. Amesema maombezi kwaajili ya viongozi yatawasaidia katika kutoogopa na kutotetereka katikaimani wakati wa kuwatumikia wananchi.

Vilevile Makamu wa Rais amesisitiza suala la utunzaji mazingira pamoja na ulinzi wa amani katika mkoa huo.

Ibada ya Asubuhi ya kawaida katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba Jimbo Kuu Katoliki Songea imeongozwa na Padre Otieno Maurice.

Oliver G Nyeriga