DRC/BENI

Chama Tawala Cha Udps Chapinga Uteuzi Wa Viongozi Wapya Watakao Ogoza Secta Ya Ruwenzori Na Beni-Mbau Kivu Kaskazini

JULAI 24, 2023
Border
news image

Joseph Kasongo STHOMBA msema ji wa chama cha UDPS wilayani Beni amesmea uteuzi wa viongozi wapya wa secta ya Beni -Mbau na secta ya Rwenzori nikama uchokozi kwani kwa viongozi hao hawastahili.hii ni baada ya kusomwa kwa tangazo la serikali Jumapili 23,2023 Mjini OICHA unao patikana kwenye kilometa Zaidi ya ishirini na tano kaskazini mwa Mji wa Beni.

Chama tawala cha UPDS cha shutumu baadhi ya watu Fulani kumdanganya Waziri katika uteuzi wa viongozi wapya wa eneo husika kama uteuzi wa JAPHET MAPATHI na mwami PASCAL BULEMO kua viongozi wapya wa sekta ya ruwenzori na Beni-mbau.

Aki hujiwa mjini OICHA, msemaji wa chama hicho JOSEPH KASONGO TSHOMBA adai kua walio teuliwa kwa uongozi huo sio wana memba wa chama Tawala chao bali wana familia wa Mutu Fulani ambaye ni mmoja wa çhama.

Washabiki wa chama hicho wa lalamikia kuto husishwa kwa karibu ama kwa mbali katika uteuzi huo wakiomba kwa Waziri wa mambo ya ndani kusimamisha kwa haraka hatua hio kwaku epuka mahafa itakayo tokea ikiwa lalamiko lao halitapewa suluhisho nzuri kwa haraka.

Germain Hassan /MTV Beni