Tanzania

Agizo La Rais Dk. Samia Latekelezwa Ngara Na Waziri Aweso Azindua Mradi Wa Maji

JULAI 24, 2023
Border
news image

Mnamo 22 Februari mwaka 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa Wilayani Ngara kwenye sherehe za maazimisho ya miaka 25 ya uaskofu wa askofu Severini Niwemugizi wa jimbo la Rulenge Ngara alumuagiza Waziri wa Maji Tanzani Mhe.Jumaa Aweso kutatua kero ya maji Ngara mjini.

Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani alitoa maelekezo haya baada ya kupokea taarifa ya changamoto kubwa ya Maji na ndani ya siku mbili 24 Februari 2022 Waziri Aweso wilayani Ngara kwa ajili kuanza hatua zakutatua changamoto ya maji na kuianza kazi mara moja.

Aidha sasa ikiwa ni kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitano pekee kupita Mradi wa Maji Ngara mjini umezinduliwa rasmi na Waziri wa Maji Mhe. Aweso alieambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng. Nadhifa Kemikimba.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amemuagiza katibu mkuu wizara ya Maji kuelekeza fedha ya kubadili Miundombinu ya usambazaji maji Ngara mjini na kuwapatia wahandisi wa Maji eneo hiki gari ili kuimarisha utendaji kazi.

Mradi huu umegharimu kiasi cha Tsh 904 na tayari unatoa maji ukiwa unahudumia wananchi 18,270.

Viongozi na wananchi wa Wilaya ya Ngara wametoa Shukrani zao za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jambo hili muhimu kwa wana Ngara kutimia kwa muda kipindi cha muda mfupi.

Waziri Aweso amehitimisha ziara yake Ngara mkoani Kagera kwa kuwapongeza sawa wahandisi wa Wilaya zote mkoa huo, Mhandisi wa mkoa na Mkurugenzi wa BUWASA kwa kazi nzuri alioishuhudia katika ziara yake.

Oliver G Nyeriga