TANZANIA

Ziara Ya Naibu Waziri Wa Nishati Mkoani Tabora Yaleta Mabadiliko

SEPTEMBA 25, 2023
Border
news image

Naibu Waziri wa Nishati nchini Tanzania Judith Kapinga amewasili mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia leo.

Mara baada ya kuwasili mkoani humo, Kapinga alipokelewa na mwenyeji wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Kenan Kihongosi, ambaye Pia ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo na baadaye kuwasili katika ofisi za Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) na kupokea taarifa kuhusu hali ya upatikanaji wa Umeme mkoani humo kutoka TANESCO na Wakala wa Nishati Vijijini( REA).

Baada ya kupokea taarifa hiyo pamoja na mambo mengine alitoa maelekezo kwa wasimamizi wa utekelezaji wa Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini.

Katika ziara hii Naibu Waziri atazungumza na wananchi wa Wilaya ya Nzega, Uyui na Urambo pamoja na kuwasha umeme katika baadhi ya vijiji vya wilaya hizo.

Hii leo atawasha umeme katika kijiji cha Ikindwa(Bukene) wilayani Nzega pamoja na kuzungumza na wananchi.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania