KENYA

Watuhumiwa wa Mauaji ya Ahalaiki ya Ashakahola Kusalia Korokoroni

SEPTEMBA 11, 2023
Border
news image

Mahakama ya Shanzu mjini Mombasa nchini kenya imeamuru washukiwa 66 wa kundi la kufanya ibada ya kujinyima chakula hadi kufa la huko shakahola kaunti ya Kilifi nchini kenya, kuzuiliwa kwa siku 30 zaidi. Hii ni baada ya afisi ya uangalizi wa sheria mjini Mombasa kuwasilisha maombi kwa mahakama kutaka muda zaidi wa kukamilisha ripoti yao.

Kulingana na afisi ya uangalizi inayoongozwa na Wycliffe Wathome, walifanikiwa kuwahoji washukiwa 63 kati ya 66 na kuongeza kuwa wengi walikuwa wagumu kutoa maelezo ya familia na washukiwa wengine hawakuwa wa asili ya Mombasa huku mmoja akiwa mgeni hivyo basi kuchelewesha ripoti ya mwisho.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Yusuf Shikanda alisema kuwa mahakama inayoshughulikia suala hilo ni jambo la busara kuomba taarifa za kifamilia kuhusu shauri hilo. Shikanda aliwataka washukiwa hao kutoa ushirikiano kwa maafisa wa uangalizi akisema kuwa maafisa hao hawaendi kwao kwani wangeona lakini taarifa wanazotafuta zinaweza kuwasaidia hata washukiwa katika kesi yao.

Washukiwa hawa ni Pamoja na kasisi wa kanisha la good news international nchini kenya Paul Makenzie, ambaye anazuiliwa kwa kuendeleza ibada hiyo ya kuwashawishi waumini wake kujinyima chakula hadi kufa ili wamuone yesu.

Kufikiasasa Zaidi ya watu 427 walidhibitishwa kufariki kwenye kanisa hilo, huku watu mia 613 wakiwa bado hawajulikani walipo. Hata hivyo watu 91 waliokolewa huku shughuli za kufukua makaburi zikiendelea.

AM/MTV NEWS