DRC - ITURI

Watu zaidi ya kumi wauwa na watu wenye silaha katika Kambi ya wavuvi ya Gobu wilayani Djugu

AGOSTI 28, 2023
Border
news image

Shambulizi lili ripotiwa jumapili Ogasti 27 , na kutekelezwa na wapiganaji wanao dhaniwa kutoka kundi la Coodeco . Ambao wali lenga kambi ya wavuvi kijijini Gobu katika maeneo ya Vendro Tarafani Bahema kaskazini wilayani Djugu . Kwa mujibu wa Pilo Mulindwa Willy mkuu kiongozi wa tarafa ya Bahema kaskazini anasema :

"Kambi na watu ni karibu karibu , kuna wana Jeshi ila ni wachache na raia wako pembezoni , wali fika na kufiatua risasi kadhaa mara moja kuanza kuingilia wavuvi , kwa sasa tuna idadi ya watu 11 ambao wame uawa kikatili . Wanajeshi wana jaribu kufuatilia wapiganaji hao , wanajeshi wa majini wali changia pakubwa ku zuia mahafa zaidi , wao ndiyo wana leta hiyo idadi ya wale watu wenye wana uawa "

Kwa swali la kufahamu kwa nini mazungumzo hai fanyike ili kujuwa Sababu na kusuhisha hili jambo .

Pilo Mulindwa Willy mkuu kiongozi wa tarafa ya Bahema kaskazini alijibu :

"Kila mara tuna tafuta amani iingie katika vijiji lakini wandugu wetu wale wanao chukua siraha wana waita wa Coodeco hawataki kusikilizana , wana fanya watu wazubae kwa mazungumzo kisha wana anza tena mauaji , wiki mbili sasa hii hatu lale salama , tuna omba tu jeshi ifanye juhudi kwa kuweza kumaliza huu mizozo "

Pamoja na hayo , kiongozi wa mashirika ya kiraia Tarafani Bahema kaskazini Bwana charité Banza , asema idadi ya watu walio poteza maisha ni 18 , sababu kuna walio jeruhiwa vikali matumaini ya wao kupona ni ndogo , uku akiomba Serkali kuanzisha opersheni maalum dhidi ya wapiganaji hao wa Coodeco .

Eriksson Luhembwe MTVDRC BENI