DRC-Beni

DRC BENI WATU WATU TANO WAUWAWA NA WATU WANAO DHANIWA KUTOKA ADF MAVIVI BENI.

news image
AM
JANUARI 25, 2024
Border
news image

Akizungumuza na MTVOLINE mmoja wa wakaazi alie ponea chupuchupu asema watu walio kuwa na silaha waliingia katika Mji wa MAVIVI kwa nyakati za jioni wakati bado wakaazi walikuwa hawaja lala.Mathe ansema jirani wake aliuwawa kwa mapanga amara watu wanao dhaniwa kuwa ADF walimuona aki nyanyua kichwa chake mwenzie yeye alijificha katika mifereji na ndio sababu ya kupona kwake.

Wakaazi wa mji mdogo wa Mavivi wanasema tukio hili ni la kwanza mara pale wanajeshi wa Uganda UPDF waliwasi wilayani Beni kuwasaka wapiganaji wa ADF.Mavivi ilikuwa miongoni mwa vijiji ambavyo tayari vilikuwa vimesha pata usalama na tukio la mauaji haya linatisha sana na kusababisha wakaazi wengine kuhama nyumba zao pasipo kupenda .wengine wakilalamikia uzaifu wa vyombo vya usalama na kupuuza taarifa toka kwa wananchi pamoja na wakulima walio toa taarifa kabla ya mauaji hayo.

MAVIVI ni Mji ambao unapatikana kaskazini mwa Mji wa Beni ambako kuna kikosi kikubwa cha MONUSCO ,MONUSCO ambao wanasema lengo lao nikulinda usalama wa wananchi wa Congo lakini bado wakiendelea kuuwawa katika uangalizi wa kikosi hicho ambacho kimefanya Zaidi ya miaka ishirini na tano mashariki mwa Congo.

Wakaazi wameomba Rais alie chaguliwa kuwapa usalama kwani walichagua kuomba usalama na kuomba vijiji ambavyo vilikuwa vimepata usalama kulindwa na jeshi tiifu kwa serikali ama na wazalendo wakiomba wananchi.

AMĀ /MTVONLONE