Miongoni mwa walio uwawa wanaume wa wili na wengine wakiwa wanawake ambao waliuwawa kwa mapanga na wengine kwa risasi katika kata Mji wa Oicha Matombo wilayani Beni usiku wa juma tatu.
Thimothe Kisusuti mmoja wa wakaazi wa Mji wa Oicga asema << waasi wanao dhaniwa kuwa ADF walingia katika kata ya Matombo ,Matombo ikiwa kata mmoja wapo wa kata zinazo patikana mashariki mwa Oicha, watu saba wameuwawa wote wakiwemo wanawake wa wili na wanaume nne, na walio jerihiwa wanapata tiba katika Hospitali kuu ya Oicha, kwa sasa raia wanashangaa kwani eneo nyingi hakuna jeshi, kwani walienda saidia vita vya M23 na hakukuwa usaidizi wa haraka, na hivi sasa wakaazi wanakimbilia sehemu ya usalama, Nyumba zimechomwa na pikpiki mbili>>
Kisusuti amesema wakaazi wanategemea jeshi tiifu kwa serikali lakini bado hali ikiendelea kuwa mbaya zaidi na kuzusha hofu kubwa. Oicha ni Mji kuu wa wilaya ya Beni ambako kumeuwa Mlimo wa CACAO na Kahawa lakini wakulima wakiuwawa mashambani kwao.
Kundi la ADF limeshutumiwa kwa muda mrefu kuhusika katika mauaji na mashambulizi ya watu na vijiji mbali mbali wilayani Beni na Lubero.
ADF imekuwa na wapiganaji wake wengi kutoka mataifa mbali mbali, ikiwemo Rwanda, Uganda, Tanzania, DRC, Afrika Kusini, Soudan na hata mataifa mengine ya Kiarabu ambako wapewa mafunzo.
Mauaji haya yanajiri wakati wakaazi wajipanga kushiriki sherehe za mwaka mpya lakini wakiuwawa kwa mapanga na Visu.