DRC - ITURI

Watu kumi na sita wame uawa kwa kushambuliwa na kundi lenyi siraha katika mgodi uitwao Shaba maeneo ya Kandoi wilayani Aru Mkoani Ituri

AGOSTI 29, 2023
Border
news image

Watu kumi na sita wame uawa kwa kushambuliwa na kundi lenyi siraha katika mgodi uitwao Shaba maeneo ya Kandoi wilayani Aru Mkoni Ituri.

Taarifa Toka Ituri zasema Shambulizi lilidumu kwa mda masaa 4 , usiku wa juma tatu Ogasti 28 kuamkia jumanne , Amesema kiongozi wa kiraia wilayani Aru bwana AWUNDU Heritier ,Heritier omeongeza kwamba hatma ya zaidi ya wachimbaji 20 haijulikani hadi sasa , kukiwa hofu ya idadi ya walio uawa kuongezeka wakati wowote , walio nusurika wali kimbilia sehemu za muto Welé na vijiji Jirani na walio jeruhiwa wali pekekwa katika hospitali ya Kandoi-Centre umbali wa kilomita 20 na eneo la tukio .

Mkuu kiongozi wa sekta ya Ndo Bwana OMU TOBARI Israel ame thibitisha shambulizi hilo mbaya . Utafahamu kwamba , Maeneo ya Kandoi yako umbali wa kilomita 400 kaskazini mwa Mji wa Bunia wilayani Aru . Duru hiyo ime dokeza kwamba wapiganaji wa kundi la Coodeco ndiyo wana nyoshewa kidole kuhusika na shambulizi hilo , kiongozi huyo anasema wanawake na hata watoto wali uwawa ama kutekwa na wapiganaji hao.

"Ili fanyika usiku hapa wali shambulia kabisa , wana uwa watu 16 kuna 16 walio umizwa , wana choma manyumba 5 na wana enda na watu wengi hatu juwe hesabu , wana Nyanganya pesa na zahabu za watu , ni kundi ya Coodeco wana tabia ya ku ingilia njia ya Walendu watsi tuna mpaka na kijiji kimoja hapo , wale wenye wana fika hapa ime onekana wana toka Walendu Djatsi kisha kuingia kwetu " Ali fafanua mkuu kiongozi wa sekta ya Ndo maeneo ya Kandoi wilayani Aru .

Eriksoson Luhembwe MTVNEWS /BENI