DRC GOMA

Watu kumi na mbili wajeruhiwa na mmoja kufariki Dunia wakati wa mlipuko wa bomu moja ilio toroka askari jeshi wa serikali kimakosa katika uwanja wa De L,unite Mjini Goma

SEPTEMBA 28, 2023
Border
news image

Alhamisi hii, Septemba 28, 2023, Bomu moja ya RPG lipnyoka askari mmoja wa serikali na kuangukia katika uwanja wa mchezo ya kandanda wa de l,Unite katika katika mwa mji wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Kulingana na vyanzo mbalimbali vyasema mtu mmoja amefariki Dunia baada ya kufikishwa katika kituo cha afya na wengine Zaidi ya Kumi kujeruhiwa vikali wakati wa tukio hili.

Bomu hiyo hiyo ilitoroka silaha ya mwanajeshi bila ya kukusudia ililipuka wakati wachezaji wa timu ya GOAL wakiwa katikati mazoezi yao ya kawaida.

Vyombo vya usalamahasa serikali Kivu kaskazini imetangaza kuwa Bomu hiyo ilitoka kwa jeshi la serikali kwa askari alie kuwa akipita bila makusudi . serikali Mkoani Kivu Kaskazini yasema watu kumi na mbili walipata majiraha akiwemo askari jeshi mmoja na kwa bahati mbaya mmoja wa wachezaji alie jeruhiwa amefariki Dunia, serikali ikiwa imechukuwa majukumu ya kulipa dawa kwa wagonjwa wote.

AM/MTVNEWS