Ni watu 25 kati yao watoto 9 ndio wameokolewa na Jeshi la Kongo FARDC usiku wa kuamkia juma nne Ogasti 22 kijijini Tingwe kinacho patikana kunako kilomita 70 kaskazini mashariki mwa Mji Beni Kivu kaskazini .
Raia walio okolewa , walitekwa na waasi katika mashambulizi mbalimbali kati ya mwaka 2016 na 2023 , Kepten Antony mwalushay msemaji wa operesheni sukula1 katika maeneo ya Beni Lubero
"Tuna dhibiti hali ya mambo tangu jana majira ya mchana , sababu askari wetu waliokuwa waki fuatilia adui wali pambana naye , tuli fanikiwa kukomboa raia walio tekwa . Askari wetu wana endelea na Doria ya vita katika eneo hilo kuelekea musituni ambako adui ali kimbilia "
kati yao kuna pia wanaume ila idadi kubwa ni wanawake ; asema Rachid MALIRO kiongozi wa Kiraia katika Mji Mdogo wa Eringeti .
"Afya yao ina dhoofika sana kwa watoto na wanawake , kuna watoto wa umri wa miaka 2 , 3 , 4 , wame eleza ya kwamba shamba ambayo ADF ilifanya katika mtandao wa barabara ya Eringeti Kainama , watoto 4 wa jamaa moja wali shuhudia kwamba Mama yao ali chinjwa kama mbuzi kwa pori , Fardc imeweza kutosha hizi jamaa zote kwa mikono ya hao wauni "
Ogasti 20, Jeshi la Fardc lilipambana tena na waasi hao kwenye mpaka wa mkoa wa kivu kaskazini na Ituri kijijini Baungatsu Luna karibu na mji wa Eringeti , watu 6 walifariki miongoni watuhumiwa adf 3 kwa mujibu wa duru za kijeshi .