DRC - BUNIA

Watu 12 wafariki Dunia na wengine zaidi kujeruhiwa baada ya ajali mbaya ya gari kutokea kwenye kijijini LATA mkoani Ituri kaskazini mashariki mwa Congo

AGOSTI 24, 2023
Border
news image

Ni Watu 12 ambao wamefariki Dunia pale Lorry iliyo kuwa ikibeba shehena kubwa la mizigo na abiria kupinduka Jumatano Ogasti 24 kijijini LATA. Umbali wa kilomita 35 kusini mwa Mji la Bunia mkowani Ituri katika mtandao wa barabara Bunia -Aveba, Abiria wengine 12 wame jeruhiwa vikali na kupelekwa hospitali kupata matibabu Mjini Bunia.

Kiongozi wa Kiraia wilayani Irumu eneo la Walendu Bindi Bwana ANDROZO Gabriel , ame dhibitisha taharifa."Ni kweli jana gari ilitokea Aveba kuelekea Bunia ikafanya ajali, pale watu wali fariki 12 waka jeruhiwa na habari tunazo sasa ni wenye wana fariki wame ongezeka. Ndani ya gari mulikuwa mizigo walikuwa waki rudi Bunia, watu wanapo tokea "Town" Bunia Wana fika huku sehemu za Geti na Aveba, wana nunua vyakula vingi sababu bey ni raisi, wana jaza mizigo mingi sana ile njo inakuwa tatizo "Bali vifo aidha majeraha kume ripotiwa pia mali nyingi kuharibika hasa vyakula na Lori kupatwa na uharibifu mkubwa, imesema duru hiyo.

Ericksson Luhembwe /MTV BENI