TANZANIA

Wasimamizi wa Miradi ya Elimu Watakiwa Kutimiza Majukumu Yao Tanzania

SEPTEMBA 20, 2023
Border
news image

Timu ya Wataalam wa Idara ya Usimamizi wa Elimu kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI pamoja na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania kwa kushirikiana na Wadau kutoka Benki ya Dunia wametoa wito kwa wasimamizi wa Miradi ya Elimu kutimiza majukumu yao ya kusimamia kwa weledi miradi hiyo.

Timu hiyo ya wataalam imefanya ziara ya kikazi ya ufuatiliaji na tathmin ya utekelezaji wa Miradi ya SEQUIP na BOOST katika Halmashuri ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.

Mratibu Msaidizi Mradi wa SEQUIP Ofisi ya Rais TAMISEMI Mwl. Robert Msigwa amesema, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mwezi juni mwaka huu imepokea kiasi cha shilingi Bil. 3 kujenga Shule ya Sekondari ya Bweni ya Wasichana ya Mkoa ambapo itakapokamilika itapunguza changamoto za kielimu kwa wasichana.

Msigwa ametoa wito kwa wasimamizi wa Miradi ya Elimu wakati wa utekelezaji wa ujenzi huo kuwa na uwazi ili kila mtu kwa nafasi yake ashirikishwe ili kujua kwenye ujenzi kinaendelea kitu gani na nafasi yake kiutendaji ipo wapi kwa kufanya hivyo itasaidia mradi huo kukamilika kwa wakati.

''miradi hii inatumia mafundi wetu wa hapa hapa Kigoma nitoe wito kamati zile zilizoainishwa kutekeleza majukumu yao zifanye kazi ili tuisaidie Serikali katika malengo yake ya kuboresha sekta ya elimu nchini" amesema Msigwa

Kwa upande wa Mratibu Msaidizi Mradi wa BOOST Ofisi ya Rais- TAMISEMI Bw. Reuben Swilla amesema timu zikishirikishwa na kila mtu akifanya kazi yake kwa weledi itasaidia kupunguza hoja za ukaguzi sababu kila mmoja atakua anajua eneo lake la kazi.

Naye Afisa Ufuatiliaji na Tathmin Mradi wa SEQUIP na BOOST Bw. Mlagilo Kafu ametoa wito kwa viongozi hao mbali ya usimamizi wa miradi lakini pia wasisahau kujikita kusimamia viashiria vya utekelezaji wa miradi ikiwemo suala la uandiakishaji na usalama.

"Tusimamie viashiria vya Mradi wa SEQUIP na Mradi wa BOOST ili tufanikiwe nilazima tusimamie kwa usawa

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania