TANZANIA

WASAIDIENI WATUMISHI MSIWABANIE FURSA - KIKWETE

MEI 06, 2024
Border
news image

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewaonya baadhi ya maafisa rasilimali watu kuhusu tabia inayoendelea ya kutowatendea vyema watumishi wenzao wanaowaongoza katika ofisi mbalimbali .

Naibu Waziri Kikwete ameyabainisha hayo Jijini Arusha kwenye mkutano wa 11 wa wananchama wa chama cha Maafisa Tawala na Rasilimali watu (AAPAM) huku akionyesha kuchukizwa na roho mbaya walizonazo baadhi ya watendaji hao akitoa mfano wa Rorya juu ya utaratibu za upandishaji madaraja.

Katika hatua nyingine Mhe. Ridhiwani amewataka maafisa Rasilimali watu kutumia mifumo ya kiutendaji kazi ili kuwezesha haki na wajibu kutolewa kwa watumishi wa umma bila upendeleo.

Amesema mafunzi hayo yamewakumbusha kuboresha utendaji kazi na utoaji haki kwa watumishi wengine kama yalivyo malengo ya mifumo hiyo ambayo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameendelea kusisitiza ufanyaji kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kuweka mazingira mazuri kwa wafanyakazi na wale wanaowahudumiwa ambao ni wananchi.

MTV Tanzania