DRC

Wakimbizi Wa Vita Mashariki Mwa Congo Waomba Amani Na Usalama Ili Warudi Kwenye Vijiji Vyao

SEPTEMBA 21, 2023
Border
news image

Wakiwa katika kambi mbali mbali pembezoni mwa Mji wa Goma kivu kasakzini wakaazi wa vijiji mbali mbali kutoka wilayani ya Rutshuru,Nyiragongo,masisi waomba serikali kurejesha amani na usalama katika eneo zao kwani kwa sasa wapitia hali mbaya ya ukosefu wa usalama ,wamesema hao wakimbizi wa vita vya M23 na jeshi la serikali wanai ishi katika hema ambazo za vuja maji pale mvua zinapo nyesha.

Solange Tuisabe mama anae kuwa na Watoto 7 alikimbia Kijiji chake cha Rubare kilometa thelathini kaskazini mwa Mji wa Goma aomba serikali kuwaondoa waasi wa M23 kwenye Kijiji chake ili arudi kwani ameshindwa sasa kuvumilia mateso wanao pitia kambini ambako hakuna hata choo kwa wanawake na Watoto.

Mji wa Goma kwa sasa una kambi Zaidi ya tisa kubwakubwa ambako wanawake wanalalamikia ubakaji,njaa,mateso na ukosefu wa huduma ya afia.wakimbizi hao wanasema Watoto wao wameshindwa kuelekea shuleni kutokana na ukosefu wa pesa wakishindwa kuwalipia karo shuleni Watoto.

Serikali ya Congo ikisema inaelewa mateso wanayo pitia Watoto na wanawake kambini na hivi karibuni suluhisho litapatina .Rais wa Congo ametangaza kwamba hawezi kufanya mazungumuzo na waasi wa M23 na M23 ikisema kumaliza machafuko mashariki mwa Congo inahitaji mazungumuzo ya kina.

AM/MTVNEWS