DRC

Wakaazi wa vijiji mbali mbali wilayani Masisi waomba serikali kuwajibika kurejesha usalama wa wananchi wanao endelea kukim bia vita vya M23 .

MEI 02, 2024
Border
news image

Baada ya waasi wa M23 kuchukuwa eneo la Madini muhimu la Rubaya na vijiji vingine ,wakaazi waomba Rais wa Comgo Felix Tshisekedi kuwasikilia huruma wakaazi wanao endelea kukimbia vijiji vyao kutokana na mapigano ya M23 na jeshi la serikali ya congo Drc Fardc .

Hii ni baada ya M23 kuchukuwa sehemu nyingine kubwa ya uchimbaji madini.na kulazimisha wakaazi kukimbia upya vijiji vyao katika uangalizi wa vikosi vya SADC na Umoja wa Matifa MONUSCO ambao wako DRC kusaidia jeshi la Congo kutwangana na M23 .wakaazi wakishangazwa kuona waasi wa M23 kuendelea kuchukuwa vijiji bila kushuhudia makabiliano makubwa na waasi wa M23 .

Rubaya ni eneo Muhimu la uchimbaji madini ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa na Rwanda na kuwa chanjo cha vita mashariki mwa Congo .Kuchukuliwa kwa Rubaya itawapa Nguvu Zaidi waasi wa M23 kununua vifaa vya kijeshi na kuwa na nguvu Zaidi kipesa .

Serikali ya Ufarasa iliomba M23 kuondoka kwa haraka katika eneo wanazo zibiti na Rwanda kuondoa wanajeshi wake kwenye ardhi ya Congo.huku vyomvo vya usalama vya DRC vikiendelea kushuhudia kurundikwa kwa jeshi la Congo kwenye vijiji vingi vya Masisi,Rutshuru na Nyiragongo kusaidia uasi wa M23 ambao umesha sababisha maelfu ya wakaazi kuwa wakimbizi wa ndani katika taifa lao.

AM/MTV DRC ONLINE