TANZANIA

Waandishi wa habari, wanasiasa, wanafunzi na viongozi wapewa mafunzo ya kupambana na utapanyaji wa taarifa za uongo (Fakenews) wilayani Lubero Kivu kaskazini

SEPTEMBA 15, 2023
Border
news image

Waandishi wa habari, wanasiasa, wanafunzi na viongozi wapewa mafunzo ya kupambana na utapanyaji wa taarifa za uongo (Fakenews) wilayani Lubero Kivu kaskazini.

"Tunaibuka wenye nguvu na karibu kubadilika kutokana na mafunzo haya ambayo yametualimisha Zaidi," alisema Mby José Mby msichana anae kuwa na miaka ishrini na saba mwanafunzi kunako Univasiti ya Saint Croix pa Mulo wilayani Lubero Kivu kaskazini kilometa Zaidi ya hamsini kusini mwa Mji wa Butembo.

Kama wanachama wengine ishirini wameshiriki , ikiwemo wawakilishi wa vyama vya siasa, wanachama wa asasi za kiraia, wasimamizi wa mitandao ya kijamii vya WhatsApp, vijana na waandishi wa Habari. Utafamu kwamba mradi huo umefanikiwa na kuandaliwa MONUSCO yaani Umoja wa Mataifa nchini DRC wilayani Lubero katika ushirikiano wa chama cha wanahabari UNPC eneo husika.

“Mafunzo hayo yalikuwa ya muhimu sana kwetu. Binafsi niliishi katika ujinga. Sikupendezwa sana na yale yaliyokuwa yakifanyika kwa ujumla, Sikujua chochote kuhusu tulichojifunza leo. Mafunzo haya yaliniruhusu kufungua macho yangu na kuwa na sura mpya ya kile kinachosemwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Mby José.

Hatari na tahadhari....

Bado katika eneo hili, washiriki wenyewe wanatambua, matokeo ya upotoshaji yanaonekana.

"Uvumi unakuja zaidi kutoka kwa vikundi vya shinikizo, pia tuna vyama vya siasa, vikundi vya WhatsApp. Maana sasa kila mtu amekuwa mwandishi wa habari: ukishakuwa na simu yako ya mkono Android, unashiriki habari bila kusoma yaliyomo bila hata kuangalia kama inatoka wapi, inatoka sehemu gani? Kwa hivyo hii inaleta idadi ya watu katika mchanganyiko,”na kuchanganyikiwa kiakili anasema David Mayanu, mshiriki wa semina.

Mnamo 2009, kwa mfano, uvumi wa kichaa ulienea hapa, ukiripoti usafiri hadi Lubero na shirika la Umoja wa Mataifa la raia wa Rwanda. Kati ya magari yaliyochomwa moto na waandamanaji waliodanganywa na wahasiriwa wa habari hii potofu, na unyanyasaji mwingine wa kimwili, "shirika za kiutu za kimataifa" ziliamua kuondoka Lubero. “Miaka kumi na nne, bado tunaishi vinyume vya hayo matokeo wakisema wahuzuriaji.

osephine Mby ameongeza "Nilielewa kuwa kwa sababu ya upotoshaji, jamii yetu inarudi nyuma katika maendeleo yake. Maendeleo ya kiakili, kijamii, kiuchumi... Nimekuwa na ndoto ya kufanya kazi katika shirika la kiutu la kimataifa. Pamoja na uvumi huu wote wa uongo, mara Monusco inapoondoka eneo hilo, shirika hizi pia zina hatari ya kuondoka. Tunakwenda kufanya kazi wapi? Je, tutawasaidiaje wazazi na familia zetu? Hii ni moja ya hatari nyingi za habari potofu."

Kwa hiyo amejikusudia kufundisha jamii wa chuo kikuu cha Mulo kuhusu hatari ya kusambaza habari potofu.

Asaph LITIMIRE