DRC

Viongozi wa mikoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo watangaza kuwazika watu Zaidi ya hamsini walio uwawa na jeshi LA SERIKALI YA DRC tarehe thelathini iliopita

SEPTEMBA 17, 2023
Border
news image

Katika tangazo lilo fikia MTV katika Mji wa Goma hii juma pili ,Msemaji wa jeshi eneo hilo ametangza kwamba mahakama Pamoja na serikali imeamua kuwazika watu walio uwawa kwa risasi wakati walipo jaribu kuandamana dhidi ya kikosi cha Umoja wa Matifa MONUSCO,wengi wao wakiwa wahumini kutoka kanisa la wazalendo ambao waliuwawa na vyombo vya usalama vya DRC kwa tuhuma kwamba waliandamana bila ruhusa ikiwa ni kukiuaka sheria za taifa.

Kwa sasa kesi ikiwa mahakamani na walio husika wote wanajeshi kutoka kikosi cha walinzi wa Rais wa Taifa hasa makanda wao ambao ndio wanashutumiwa kuwa walitumia vibaya jeshi,silaha na risasi na kukiuaka haki za binaadamu.

Utafahamu kwamba mili ya watu walio uwawa kwa sasa ipo katika hali mbaya ,ikiwa imeharibika,familia zikiomba serikali kusaidia maziko yao na kusaidia familia za watu walio uwawa bado mahakama ikiwa haija toa humu.

AM/MTV NEWS - MTV Tanzania