KENYA

Uchumi wa Kenya Ulikua kwa Asilimia 5.4 Katika Robo ya Pili ya Mwaka Huu Ikilinganishwa na Ukuaji wa Asilimia 5.2 Katika Kipindi Sawia Mwaka 2022

OKTOBA 06, 2023
Border
news image

Uchumi wa Kenya ulikua kwa asilimia 5.4 katika robo ya pili ya mwaka huu ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 5.2 katika kipindi sawia mwaka-2022. Shirika la kitaifa la takwimu limesema ukuaji huo ulichangiwa na kuimarika kwa sekya ya kilimo. Aidha shirika hilo limesema sekta ya kilimo iliandikisha ukuaji wa asilimia 7.7 katika kipindi hicho. Katika kipindi hicho, viashirio vingi vya uchumi kwa jumla vilionyesha ukuaji wa biashara ndogo huku riba ya mikopo ya benki kuu ikipanda hadi asilimia 10.50 kutoka asilimia 9.50. Mfumko wa bei ulifikia kiwango cha wastani cha asilimia 7.15 katika robo ya pili ya mwaka-2022 hadi asilimia 7.94 katika robo ya pili ya mwaka-2023 hasa kutokana na bei ya juu ya chakula na mafuta. Shilingi ya Kenya ilishuka thamani dhidi ya sarafu nyingine za kigeni huku ikishuka kwa asilimia 20.2 dhidi ya Yuro, asilimia 18 dhidi ya Dola ya Marekani na asilimia 17 dhidi ya Pauni ya Uingereza. Shilingi ya Kenya pia ilipoteza thamani dhidi ya shilingi ya Uganda na Tanzania.

AM/MTVNEWS - MTV Tanzania