TANZANIA

Timu ya Majadiliano Kuchakata na Kusindika Gesi Asili Yapongezwa - Dk. Biteko

SEPTEMBA 12, 2023
Border
news image

Dkt. Biteko aipongeza Timu ya Serikali ya Majadiliano kuhusu mradi wa kuchakata na kusindika Gesi Asilia (GNT)

Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amekutana na Timu ya Serikali ya Majadiliano kuhusu mradi wa kuchakata na kusindika Gesi Asilia (GNT) ili kufahamu hatua zilizofikiwa kuhusu majadiliano hayo.

Dkt. Biteko amekutana na timu hiyo katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza timu hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya hadi hatua iliyofikiwa mpaka sasa.

Katika kikao hicho Dkt. Biteko ameielekeza GNT kukutana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikiali, Inaoshughulika na mikataba ili kuwaeleza kwa kina maendeleo na hatua iliyofikiwa hadi sasa.

Dkt. Ameitaka Timu kuwa huru katika kupokea mawazo kila mmoja katika kujenda uelewa wa pamoja .wanapofanya kukubaliana mambo.

Ametaka timu hiyo kuongeza kasi ili kukamilisha majadiliano hayo ili mradi huo uanze kutekelezwa kwa kuwa wananchi wanausubiri kwa hamu kubwa kutokana na umuhimu wake kwao na Taifa kwa jumla.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini, Musa Makame na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Petrol Lyatuu na viongozi wengine kutoka Wizara ya Nishati.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania