TANZANIA

Tamisemi Queens Tanzania Mmetuheshimisha - Dkt. Mahera

SEPTEMBA 10, 2023
Border
news image

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania Dkt.Charles Mahera ameipongeza timu ya TAMISEMI QUEENS kwa kuwa mabingwa mashindano ya Ligi ya Muungano kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo tangu mwaka 2021 hadi 2023.

Dkt. Mahera ameyasema hayo Jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwenye hafla fupi ya kuwapongeza wachezaji iliyofanyika katika Ofisi ya Rais -TAMISEMI

Amesema kuwa Ofisi ya Rais -TAMISEMI inatambua mchango mkubwa wa TAMISEMI SPORTS CLUB na TAMISEMI QUEENS mbali tu ya michezo pia kupita michezo hiyo wanasaidia kuitangaza Wizara.

“Ushindi huu ni wa Rais sababu Wizara hii ni ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hiyo kombe hili ni muhimu kwa Wizara "amesema Dkt. Mahera

Amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kushirikiana nao kwa karibu ili kuhakikisha timu hiyo inashiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Amewataka kuendelea kuwa na ushirikiano hasa katika kipindi hiki cha kujiandaa na mashindano ya SHIMIWI yatakayofanyika mwezi Septemba mwaka huu Mkoani Iringa.

Naye, kiongozi wa Msafara Yabes Katamba amesema, jumla ya mechi kumi walizocheza zote walishinda na kufanikiwa kupata magoli 467 kati ya magoli 527 lakini pia kufanikiwa kupata pointi zote 20 walizotakiwa kuzipata ikiwa ni washindi wa kwanza na pointi 18 walipata KVZ.

Amesema mchezaji wa TAMISEMI QUEENS Lilian Jovin aliibuka na ushindi wa mchezaji bora ambae aliweza kufunga magoli 467 huku mlinda mlango bora aliibuka Mereciana Kizeba ameeleza timu walizopambana naza ni pamoja na Mafunzo ZNZ, JKU, ZNZ, NSSF DSM, JESH STAR,Uhamiaji DSM,JKT DSM,Zimamoto ZNZ,ZNZ worries,KVZ na Polisi Arusha.

Awali akisoma taarifa Mwenyekiti Msaidizi Saida Marijani amesema timu hiyo imekua na umoja pamoja na ushirikiano wa wachezaji na viongozi ndio mana kwa mara ya tatu mfululizo imekuwa kitwaa ubingwa wa kombe hilo.

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania