DRC

Shirika La Raia Katika Mji Wa Butembo Laomba Raia Kuwa Waangalifu Wakati Huu Wa Mapigano Makali Kati Ya M23 Na Jeshi La Serikali FARDC

DESEMBA 18, 2024
Border
news image

Mathe Saanane mkuu kiongozi wa mashirika ya kiraia katika Mji wa Butembo aomba wakaazi kuwa waangalifu .Mathe amesema hayo hii juma tarehe nne decemba wakati wa mahojiano na wanahabari. Hii ikiwa baada ya kushuhudia wimbi jipya la wakaazi kuwasili Mjini wakitoroka mapigano kati ya M23 na jeshi la serikali ya Congo FARDC, na kuchukuwa miji kadhaa ikiwemo alimbongo ,Vutsorovya na Matembe.

Butembo ni mji wa kibiashara jwa historia yake na waaazi wake wakiwa na juhudi kubwa katika kilimo na ufugaji MATHE SAANANE mratibu wa shirika la kiraia akiomba wananchi wote kuendelea kuunga mkono jeshi tiifu kwa serikali .

Viongozi wa wapiganaji wa chini kwa chini wazalendo, wakiombwa uungwaji mkono ,Hassan ni mmoja wa makamanda wa wazalendo katika Mji wa Butembo

Hayao yana jiri wakati hali ni ya wasiwasi nay a kutatanisha wilayani lubero ambako jeshi la congo FARDC lapambana vikali na M23 ambayo imechukuwa vijiji kadhaa wilayani Lubero na kusababisha wakaazi wengi kuwa wakimbizi ndani ya taifa lao wakikimbilia katika mji wa Butembo ,Lubero na wengine kwenye vijiji

Ripoti yake Kambale Sivanzire serge akiwa katika Mji wa Butembo.

Kambale Sivanzire serge - AM/MTV News DRC