KENYA

Serikali ya Kenya Imeanzisha Uchunguzi Kuhusiana na Ugonjwa Usiojulikana Uliowakumba Wanafunzi 95 wa Shule ya Upili Magharibi Mwa Taifa la Kenya

OKTOBA 04, 2023
Border
news image

Serikali ya Kenya Imeanzisha Uchunguzi Kuhusiana na Ugonjwa Usiojulikana Uliowakumba Wanafunzi 95 wa Shule ya Upili Magharibi Mwa Taifa la Kenya Karibu na Taifa Jirani la Uganda. Zaidi ya Wanafunzi 90 Wamelazwa Hospitalini, Huku Kukiwa na Hofu ya Wanafunzi Zaidi Kuambukizwa. Shule Hiyo Tayari Imefungwa

Mamlaka ya afya nchini Kenya inachunguza ugonjwa usiojulikana baada ya zaidi ya wanafunzi 90 wa shule za upili ya eregi kulazwa katika hospitali mbalimbali za kaunti ya Kakamega, Magharibi mwa Kenya. Wanafunzi walikuwa na dalili za maumivu ya goti na walikuwa na ugumu wa kutembea.

Afisa mkuu wa Wizara ya Elimu ambaye alitembelea shule hiyo aliwaambia wazazi waliokuwa na wasiwasi kwamba hali imedhibitiwa.Alisema wanafunzi wengine watasalia shuleni. Hata hivyo jioni ya leo, mamlaka ya afrya imeagiza shule hiyo kufungwa kwa muda usiojulikana, hali inayoashiria kuongezeka kwa ugonjwa huo.

Sampuli za damu, zilitumwa kwa maabara katika KAUNTI jirani ya Kisumu na mji mkuu, Nairobi. Matokeo ya mwisho ya kubaini chanzo cha ugonjwa huo yanatarajiwa baadaye kesho Kutoka Jijini Nairobi nchini Kenya.

Dennis Chisaka