DRC
Serikali ya congo yakataa mazungumuzo ya moja kwa moja na M23
DESEMBA 19, 2024
Akizungumuza na wanahabari Mjini kinshasa waziri wa habari wa DRC Patrick Muyaya asema “Si kukosekana kwa Rais wa Rwanda kule Luanda wala kuwepo kwa majeshi yake Mashariki ambako kutatufanya tufikirie upya msimamo wetu ambao uko wazi kabisa."
"Hatutawahi kujadiliana na M23!. "Majadiliano yaliyopangwa na makundi yenye silaha yatafanyika ndani ya mfumo wa mchakato wa Nairobi."
"Rais Kagame ndiye baba wa kweli na mamlaka ya maadili ya vuguvugu la kigaidi la M23! Mashine ya kudanganywa haiwezi kufanya kazi kila wakati.
Asema Patrick Muyaya masemaji wa serikali ya kinshasa.