DRC GOMA - KIVU KASKAZINI

Serikali ya Congo ya Mtimua Gavana Mmoja wa Kijeshi Mashariki mwa Congo na Kumteua Mwingine

SEPTEMBA 20, 2023
Border
news image

Baada ya watu Zaidi ya hamsini kuwawa na vyombo vya usalama tarehe thelathini ogasti iliopita,serikali ya DRC kupitia hatua ya Rais wa Congo Felix Tshisekedi imemsimamisha kazi gavana wa kijeshi Kivu kaskazini Luteno Generali Constan Ndima ,kwa tuhuma za kushindwa kuzuia vitendo vya kialifu Mjini Goma.

Gavana huyu amegombelewa na Meja generali Piter Cirimwami Kuba ambae ndie atahusika na operesheni za kijeshi na uongozi wa Mkoa wa Kivu Kaskazini mwa muda.

Wakaazi wa Mkoa huu hasa kutoka eneo ambazo zipo mikoni mwa waasi wa M23 wakiomba serikali kuondoa M23 na kurejesha amani kwenye vijiji vyote ili walime shamba zao kuliko kubaki katika kambi kwa Muda mrefu ambako wapitia hali ngumu na mbaya ya kimaisha.

Utafahamu kwamba mikoa ya kivu Kaskazini na Ituri ipo mikoni mwa magavana wa Kijeshi lakini mikoa hiyo ikiendelea kushuhudia ukosefu wa usalama ikiwmo mauaji na ukiukwaji wa haki na msingi ya binaadam.wananchi wa mikoa hiyo wakiomba Rais wa Congo kuhudumisha amani ilio potea kwa muda mrefu.

M23 imekuwa ikomba mazungumuzo na serikali lakini serikali kwa upande wake nayo ikisema haiwezekani kwa sasa kuzungumuza na M23 ambayo imeweka uongozi wake katika wilaya ya Rutshuru,Bunagana,rutshuru,kiwanja na sehemu moja ya wilaya ya masisi na Nyiragongo.

AM/MTVNEWS - GOMA