DRC GOMA

Serikali ya Congo DRC yaanzisha uchunguzi kuhusu sababu ya mauaji ya wahumini wa kanisa la wazalendo Mjini Goma Kivu Kaskazini tarehe 30 uliopita

SEPTEMBA 3, 2023
Border
news image

Waziri wa mambo ya ndani Pamoja na wazjumbe wengine kutoka serikali ya Kinshasa waliwasili juma mosi usiku katika Mji wa Goma ,ambako wamewasili kwa ajili ya kuwasikiliza wakaazi,wahumini wa kanisa la wazalendo,mashirika ya kiraia na vijana wengine Pamoja na vyombo vya usalama kuhusu sababu kubwa la utumiaji wa silaha na nguvu za kupindukia kuzima maandamano ulio kuwa imepangwa na wahumini wa kanisa la wazalendo Mjini Goma.

Maandamano ulio kuwa ikilenga kuifukuza MONUSCO kwa tuhuma kwamba MONUSCO imeshindwa kulinda raia wa Congo.vyombo vya usalama vilishutumu wahumini kukiuka na kukaidi amri ya serikali na kutaka kuleta Vurugu Mjini Goma.

Ujumbe wa serikali umetembelea eneo la tukio Nyabushongo Pamoja na baadhi ya Hospitali ambako wamelazwa wangonjwa walio jeruhiwa kwa risasi na jeshi la serikali.

Serikali ilitangaza kuwa watu Zaidi ya Arbaini waliuwawa na wengine Zaidi ya thelethini kujeruhiwa na wengine kukamatwa Zaidi ya miamoja hamsini.

Kanisa ya wazalendo imekuwa na msingi wa mababu yaani mila za kiafrica,ikifundisha watu kuwa wazalendo na vijana kuepuka kutumiwa na mataifa ya magharibi wala kudanganywa na kuepuka ulevi wa utumiaji Pombe kali.

Mahakama ya kijehsi ilianzisha kesi ya wahusika hii ijuma na kuanza kuwasikiliza watu walio kamatwa wakati wa purukushani,hadi sasa bado mahakama ikiendelea kufahamu kwanza wahusika kabla ya kuendelea na kesi kamili.

Serikali ime ahidi kutangaza ukweli kwani tukio hili ni mbya na ngumu kwa walio poteza familia wao na wahusika wataadhibiwa.

AM /MTVNEWS