DRC

Serikali ya Congo DRC na ile ya Burundi yaweka makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na vyombo vya usalama.Makubaliano hayo yameafikiwa Mjini Kinshasa

AGOSTI 29, 2023
Border
news image

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi imekubaliano kushirikiana kiusalama na kijeshi kwa ajili ya usalama kwenye mataifa yao mawili.maafikiano hayo yamefanyika Mjini Kinshasa ambako Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye nae Felix Tshisekedi wa Congo DRC wameomba kikosi cha Africa mashariki kuwajibika na kulazimisha waasi wa M23 kusalimisha silaha zao ,Rais wa Congo ameomba wanajeshi kutoka mataifa mengine ya Africa mashariki kuiga mfano wa kikosi kutoka Burundi ambacho kinajaribu kuzuia waasi wa M23 wanao taka kuchukuwa maeneo mengine ,huku wanajeshi kutoka Kenya,Soudan Kusini na Uganda wakialaumiwa kushirikiana na M23 na hata kufanya sherehe za Pamojo eneo la Rutshuru wakaazi wakithibitisha .

Makamanda wa UPDF na wale wa M23 wamekuwa wakionekana Pamoja wakitumia Mvinyo na kushirikiana na M23 japokuwa waliombwa kulazimisha M23 kuondoka wakisema wakaazi walio zungumuza na MTVNEWS.

Mbali na mkutano kuhusu hali ya usalama mashariki mwa Congo ma Rais wa wili wameweka makubaliano wa kijehsi na vyombo vya usalama kati ya mataifa mawili.

Wote wakiomba kikosi kutoka Africa mashariki kulazimisha M23 kusalimisha silaha ,swala ambalo pengine litakuwa ngu kutekeleza kulingana na uhusiano ulieko kati ya baadhi ya vikosi hivyo na mataifa inayo unga mkono M23

MTVNEWS