TANZANIA

Temesa Mpya Inayotoa Huduma Bora Inakuja: Bashungwa

OKTOBA 04, 2023
Border
news image

Serikali ya Tanzania itaongeza upatikanaji wa gesi ili kufidia mapungufu ya hali ya upatikanaji wa umeme nchini unaochangiwa na upungufu wa maji kwenye mabwawa yanayozalisha umeme.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Mashaka Biteko wakati alipotembelea mradi wa bwawa la kufua umeme la Mtera ili kujionea hali ya maji kwenye bwawa hilo ambalo limeathiriwa na hali ya upungufu wa maji unaosababishwa na ukame kutokana na kuchelewa kwa mvua .

Mhe. Dkt. Biteko alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na TANESCO itahakikisha inafanya kila linalowezekana kubuni vyanzo vipya ya upatikanaji wa umeme ikiwa ni pamoja na gesi ya kutosha ili kuhakikisha umeme unapatikana ili shughuli za kiuchumi zisiathirike kwa kukosekana kwa umeme.

"Tahadhari zilizo ndani ya uwezo wetu tunapaswa kuzichukua ikiwa ni pamoja na kulinda vyanzo vya maji na kuhakikisha wananchi wanapata umeme" Alisema Mhe. Dkt Biteko

Alisisitiza kuwa uchumi wa wananchi wa Tanzania unategemea sana upatikanaji wa umeme, hivyo shughuli zozote za kimazingira zikiathiriwa, zinaathiri pia hali ya upatikanaji wa umeme na kuwataka wananchi kutunza vyanzo vya maji.

"Serikali inakuja na mkakati wa pamoja na wadau wa maji na mazingira wakiwemo Tamisemi, Wizara ya maliasili, TANESCO, wananchi na wengineo ili kutunza vyanzo vya maji na mazingira kwani vinategemewa kwenye kuzalisha umeme

Naibu waziri mkuu Mhe.Dkt Doto Biteko alitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo jengo la mitambo yaani power house, pamoja na eneo la bwawa la kuzalisha umeme la Mtera.

Pia, ziara hiyo imehudhuriwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mha. Innocent Luoga na Mkurugenzi wa Shirika la umeme Tanzania Mha. Gissima Nyamo Hanga pamoja na Watendaji wengine kutoka shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Oliver G Nyeriga - MTV Tanzania