DRC /Kivu Kaskazini:

serikali yatangaza mazishi ya waathiriwa wa milipuko ya mabomu huko Bulengo na Mugunga Jumapili hii, Mei 12.

MEI 10, 2024
Border
news image

Wakati wa mkutano ulio shirikisha mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini Meja generali Peterv Cirimwami , serikali ya Congo kupitia waziri wa haki za binaadamu Albert FABRICE PUELA ametanga kwamba Mei 12, mazishi "ya heshima" ya wahasiriwa wa milipuko ambayo ililenga watu waliohamishwa kwenye kambi za Bulengo mnamo Mei 3 karibu na Goma. ya M23/RDF Watazikwa rasmi asema Puela Ijumaa hii, Mei 10.

Katika ujumbe huu rasmi Fabrice Puela alisisitiza kuwa lengo la ziara yao GOMA ni kuunga na familia za wahanga wa janga hili. Pamoja na kutangaza idadi rasmi ya watu walio fariki Dunia ikiwa inaongezeka kutoka 14 hadi 35 waliokufa na 37 kujeruhiwa.

Miongoni mwa wahanga wa mashambulizi hayo ya mabomu ni watoto, wanawake na wazee. “Mipango yote imefanywa kwa ajili ya kuandaa mazishi yenye heshima”asema Puela.

Kumbuka kuwa idadi ya watu walio fariki Dunia tokana na milipuko iliongezeka kutoka 14 hadi 35 waliokufa na majeruhi 37 ambao walikuwa wakihudumiwa na serikali ya Kongo.

Puela akiungana na mwenzie Modeste Mutinga amesema watu hao watazikwa Nyiragongo ambako wakaazi waombwa kushiriki mazishi ya kihistoria kuwa taifa jirani la Rwanda ndilo limehu.wabuge wakiomba Rwanda kufikishwa mahakamani kuunga mkono uhalifu na mauaji mashariki mwa Congo asema Munyomo Patrick Mbunge wa Goma.

Daniel Bisongo